Jeshi la Uganda linachunguza tukio la mlinzi mmoja wa rais Yoweri Museveni kumpokonya silaha mwenzake usiku wa jumamosi na kumuua kwa kumpiga risasi mara kadhaa mwanajeshi mwenzake ndani ya Ikulu ya nchi hiyo.
Kufuatia tukio hilo wanajeshi wengine walijibu mapigo kwa kumshambulia kwa kumfyatulia risasi mwanajeshi aliyempiga risasi mwenzake na kumuua nae pia.
Wanajeshi hao ni wa kikosi maalum cha SFG, ambacho ni maalum kwa ajili ya kumlinda Rais Yoweri Museveni.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni