Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
limepiga kura ya kutuma kikosi imara cha askari 12,000 katika nchi ya
Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw.
Ban Ki-moon ameonya kuwa wanaoondesha vitendo vya mauji ya kidini
pamoja na ukatili wa kingono hawataachwa bila ya kuhukumiwa.
Umoja wa Mataifa pia umeridhia vikosi
2,000 vya wanajeshi wa Ufaransa kufanya kazi pamoja na vikosi vya
Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni