Marekani imeishutumu Urusi kwa kutumia
gesi kama kigezo cha kuibana Ukraine na nchi nyingine ili ziweze
kutii maamuzi yake.
Kauli hiyo ya Marekani imekuja baada ya
Urusi kuzionya nchi za Ulaya kuwa itazikatia huduma ya gesi kutokana
na deni la nchi ya Ukraine.
Katika hatua nyingine vikosi vya Nato
vimetetea picha za uhakika za setelaiti zinazoonyesha vikosi vya
Urusi vikikusanyika kwa wingi kwenye mpaka wa Ukraine katika wiki za
hivi karibuni.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni