.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 11 Aprili 2014

KATIBU MKUU WA CCM KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYANI BUHIGWE KWA KUKAGUA MPAKA WA TANZANIA NA BURUNDI

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia mto Malagalasi ambao ni mpaka kati ya Tanzania na Burundi alipokuwa katika ziara wilayani Buhigwe mkoani Kigoma leo Alhamisi, Aprili 10, 2014. Kinana yupo katika ziara ya siku tano mkoani humo ya kukagua uhai wa Chama na kusikiliza kero za wananchi mkoani humo. Moja ya kero kwenye mpaka huo unaokutanisha vijiji vya Kibande (Tanzania) na Murambi (Burundi) ni Watanzania kulazimika kukumbana na adha ya kuvuka mto huo kwenda kufanya biashara na kununua mahitaji kwenye soko lililopo upande wa Burundi. Wapili kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

Kinana akitazama mpaka huo na namna wananchi walivyokuwa wakivuka na wengine kushwa kwenye mto wa Malagarasi wakitoka Burundi kuingia Tanzania.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa pembezoni mwa mto Malagarasi, mpakani mwa Tanzania na Burundi wakati wa ziara hiyo.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni