.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 12 Aprili 2014

JUMUIYA YA MTAKATIFU RAFAEL, PAROKIA YA SINZA YAWAKUMBUKA WAZEE, WATOTO NA WASIOJIWEZA WANAOLELEWA KATIKA KITUO CHA NUNGE KIGAMBONI

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mtakatifu Rafael Parokia ya Sinza Mama Maria Mama wa Mkombozi, Daudi Machumu akiongea jambo na kuwatambulisha wana jumuiya alioongozana nao kwa Afisa ustawi wa jamii ( hayupo pichani ) ambaye ndiye msimamizi mkuu wa kituo cha kulea wazee na wasiojiweza cha Nunge Kigamboni jijini Dar es Salaam
 Afisa Ustawi wa Jamii Bw Moses Gunza akiongea na wana jumuiya ya Mtakatifu Rafael Parokia ya Sinza Mama Maria Mama wa Mkombozi waliofika katika kituo cha kuwalea wazee na wasiojiweza cha Nunge Kigamboni jijini Dar es Salaam kutoa misaada mbalimbali kwa ajili ya wahitaji hao. Pembeni yake ni Katibu wa Jumuiya hiyo Silvanus Mayenga. Katika maelezo yake, Gunza alisema kituo hicho kinawatunza wahitaji zaidi ya 115 wakiwemo wazee, wenye ukoma, watoto na wengine wenye ulemavu wa aina mbalimbali
 Baadhi ya misaada iliyowasilishwa kituoni hapo ikiwa ni pamoja na vyakula vya aina mbalimbali, mafuta ya kupikia, sabuni za kuogea na kufulia na nguo za aina mbalimbali kwa ajili ya wazee na wasiojiweza wanaoishi katika kituo hicho wakiwemo watoto yatima
 Mzee Robert Wile , mmoja wa wana jumuiya ya Mtakatifu Rafael akiongea na mmoja wa watoto wanaolelewa kituoni hapo
 Makamu Mweneyekiti, Jumuiya ya Mtakatifu Rafael Parokia ya Sinza Mama Maria Mama wa Mwokozi, Justin Nyenza akisalimiana na mmoja wa wazee wanaolelewa kituoni hapo
 Anna Shumbusho, mmoja wa wanajumuiya ya Mtakatifu Rafael Parokia ya Sinza akiongea na mmoja wa akina mama mwenye ukoma anayeishi katika kituo hicho cha Nunge
 Deogratius Rweyunga, mwana jumuiya ya Mtakatifu Rafael akitaniana na mmoja wa wazee wanaoishi katika kituo hicho
 Katibu wa Jumuiya ya Mtakatifu Rafael, Slivanus Mayenga akifurahia jambo na mmoja wa akina mama wanaolelewa katika kituo hicho
 Mmoja wa wazee waolelewa katika kituo cha kulea wazee na wasiojiweza, akibadilishana mawazo na Deogratius Rweyunga wakati Jumuiya ya Mtakatifu Rafael, Parokia ya Sinza walipotembelea kituo hicho mapema leo
                                                      Hii ni Zahanati iliyopo katika kituo hicho

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni