Vinara wa Ligi kuu nchini Uingereza, Liverpool, Chelsea, Manchester City na Arsenal wao watakuwa mapumzikoni pale ligi hiyo itakapoendelea leo katika viwanja sita tofauti kwa kuishuhudia Crystal Palace ambayo katika msimamo ipo nafasi ya 14 ikishuka dimabani kucheza na Aston Villa ambayo katika msimamo wa ligi kuu Uingereza ipo katika nafasi ya 13, zote hizi zikiwa na pointi 34 lakini zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.
Mechingine hii leo Fulham watakuwa nyumbani kucheza na Norwich, wao Southampton watawalika Cardiff, wakati ambapo Stoke watateremka uwanjani kucheza na Newcastle.
Wenyewe Sunderland ambao niwa miwisho katika msimamo na wanatiketi ya kuteremka daraja msimu ujao, leo wanacheza na Everton ambayo ipo katika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu.
Mchezo mwingine wa leo ni kati ya West Brom dhidi ya Tottenham.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni