Abiria wakishuka kwa dharura ( kutumia ngazi kama inavyonekana ) kutoka katika ndege ya Shirika la Ndege la Kenya ( KQ ) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere leo mchana baada ya ndege hiyo kutua nje ya njia rasmi ya kutua na kurukia ndege.
Sababu ya ndege hiyo kutua nje ya njia yake ni kutokana na mvua kubwa zilizoendelea kunyesha katika jiji la Dar es Salaam hivyo rubani kushindwa kuona vizuri.
Hali hiyo ilisababisha ndege nyingine zilizokuwa zinapaswa kutua au kupaa kuzuiwa kwa muda. Taarifa toka uwanjani hapo zinasema hakuna madhara yeyote kwa binaadamu, zaidi ya injini ya kulia ya ndege hiyo kupata hitilafu
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni