Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
akiwahutubia kwa ufupi wakazi wa mji wa Karema mkoani Katavi usiku
huu mara baada ya kuwasili akitokea mkoani Kigoma kwa boti na
kusafiri nayo ndani ya ziwa Tanganyika takribani kwa masaa kumi na
manne.Kutokana na safari hiyo kuwa ndefu ya majini,inaelezwa kuwa
kuna baadhi ya Watu wamedai msafara wa Katibu Mkuu huyo,Kinana
umepotea ziwa Tanganyika,jambo ambalo si la kweli na la kizushi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
akiwapungia wenyeji wake (hawapo pichani) waliofika kumpokea usiku
huu kwa boti akitokea mkoani Kigoma katika bandari ya Karema mkoani
Katavi,ambako amemaliza ziara yake ya siku tano na kuhamia mkoani
Katavi ambako pia atakuwa na ziara ya siku nne
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanal Mstaaf
Issa Machibya akishuka kwenye boti usiku huu kwenye bandari ya Karema
mkoani Katavi akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,na
Viongozi wengine wa Taifa,Mkoa na Wilaya tayari kwa kuanza ziara ya
siku nne mkoani Katavi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
akishuka kwenye boti wakati wenyeji wake (hawapo pichani) walipokuwa
wakimsubiri kumpokea usiku huu akitokea mkoani Kigoma katika bandari
ya Karema mkoani Katavi,ambako amemaliza ziara yake ya siku tano na
kuhamia mkoani Katavi ambako pia atakuwa na ziara ya siku nne.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni