.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 14 Aprili 2014

MUHIDIN MAALIM GURUMO KUZIKWA KESHO KIJIJINI KWAO MASAKI KISARAWE

Mwanamuziki Muhidin Maalim Gurumo ( kulia ) akiwa na mwanamuziki mwenzake Said Mabera  
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Jakaya Mrisho Kikwete akimvisha nishani Muhidin Maalim Gurumo kuenzi mchango wake mkubwa katika muziki wa dansi nchini

Mwanamuziki Muhudin Maalim Gurumo aliyefariki dunia jana katika hospital ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam atazikwa kesho jumanne badala ya leo kama ilivyokuwa imetangazwa hapo awali kijijini kwao Masaki wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.

Gurumo amefariki akiwa na umri wa miaka 73 hadi anastaafu muziki alikuwa na bendi ya Msondo Ngoma Music Band " Baba ya Muziki '. Pia alipata kuimba katika bendi za Sikinde, Orchestra Safari Sound " OSS "

Kabla ya kupelekwa kijijini Masaki kwa mazishi, Gurumo "Kamanda" kama alivyoitwa na mashabiki wake kwanza ataagwa nyumbani kwake Mabibo External. 

Meneja wa Msondo Ngoma, Kibiriti amesema huu ni msiba mkubwa si tu kwa familia ya Maalim Gurumo, bali ni msiba kwa taifa zima kutokana na tungo mbalimbali alizopata kutunga Gurumo zenye kuelimisha jamii. 

Amesema awali ilikuwa maziko yafanyike leo, lakini sasa yatafanyika kesho jumanne japo hakufafanunua zaidi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni