Waziri Mkuu wa Korea Kusini Chung-Hon won ( mwenye miwani ) akiwa amezungukwa na walinzi wake baada ya kupigwa na chupa ya maji na ndugu wenye hasira kufuatia kuzama kwa kivuko kilichokuwa na abirai 470 na mpaka sasa jumla ya watu 300 bado hawajaonekana.
Waziri mkuu huyo alikuwa amefika kuwapa pole ndugu waliokuwa wakisubiria kupata taarifa za maendeleo ya zoezi la uokoaji linavyoendelea
Mmoja wa ndugu waliozama katika kivuko huko Korea Kusini ( kulia ) akimzaba kibao mmoja wa maofisa wa serikali
Juhudi za uokoaji ziliendelea hadi usiku kufuatia kuzama kwa kivuko hicho kilichokuwa kinaelekea katika kisiwa cha Kusini cha Jeju. Hadi jana jumla ya watu wanne walikuwa wamefariki dunia, na watu wengine 167 walikuwa wameokolewa huku 300 wakiwa bado hawajaoonekana
Ndugu wa waliozama na kivuko hicho wakiwa katika juhudi za kuwatafuta ndugu na jamaa zao, japo hali mbaya ya hewa ilikuwa ni kikwazo kikubwa
Waokoaji wakiwa katika zoezi la uokoaji
Mmoja wa ndugu waliozama na katika kivuko hicho akilia kwa uchungu baada ya ndugu yake kutokuwa mmoja wa waliookolewa mpaka sasa
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni