.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 17 Aprili 2014

TISHIO LA BOMU LACHELEWESHA SAFARI YA NDANI YA SHIRIKA LA NDEGE LA MAREKANI

 Ndege ya shirika la ndege ya Marekani jana jioni ilichelewa kuruka kwa muda kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa JFK kuelekea Washington baada ya mmoja wa husika na usalama wa ndege hiyo kuona ujumbe kupitia akaunti ya Twitter ya shirika hilo, kuwa kuna bomu ndani ya ndege hiyo
Ndege hiyo namba 5714 ilikuwa imepangwa iruke kutoka uwanja wa kimataifa wa John F. Kennedy saa 1:35 usiku na abiria wakiwa tayari wameingia ndani ya ndege hiyo tayari kwa safari, ndipo ujumbe huo ulipoonekana saa 1:05, dakika 25 kabla ya ndege kuruka. 

Abiria wote 49 walikuwa salama na upekuzi ulifanywa upya kwa abiria wote pamoja na mizigo yao. Hata hivyo hakuna bomu lililopatikana, na ndege hiyo iliruka saa 3:19

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni