.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 17 Aprili 2014

LIGI KUU UINGEREZA, MANCHESTER CITY YABANWA NA SUNDERLAND USIKU WA KUAMKIA LEO

 Timu ya soka ya Manchester City imeanza kutibuliwa harakati zake za kuutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza, baada ya usiku wa kuamkia leo kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Sunderland ambayo katika msimamo wa ligi ipo mkiani ikiwa na pointi 26.
 Katika mchezo huo ambao ulikuwa muhimu kwa Man City ambayo inazikimbiza Liverpool na Chelsea, ilijikuta ikianza mchezo kwa kasi na kujipatia bao la kuongoza kunako dakika ya ya pili tu ya mchezo kupitia kwa Fernandinho bao ambalo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika. 

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Sunderland walifanikiwa kusawazisha dakika ya 73 kupitia kwa Wickham, na dakika tano baadaye Wickham akafunga bao la pili. Manchester City iliwachukua hadi dakika ya 88 kusawazisha bao hili kupitia Nasri na matokeo kuwa 2-2
Kwa matokeo hayo Man City wameendelea kubaki nafasi ya tatu wakiwa na pointi 71 nyuma ya Chelsea walio nafasi ya pili na pointi 75, wakati Liverpool wapo kileleni na pointi 77. 

Katika mchezo mwingine wa ligi kuu Uingereza usiku wa kuamkia leo, Everton wamejikuta wakifungwa mabao 3-2 na Crystal Palace

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni