Mwendesha mashtaka katika kesi ya
mauaji inayomkabili Oscar Pistorius ametoa pendekezo kuwa mwanariadha
huyo wa Afrika Kusini anatumia ushawishi wa kuonyesha hisia kama
kigezo cha kujinasua.
Pistorius aliangua kilio mara nne hii
leo na pia alitapika mahakamani, jambo ambalo mwendesha mashtaka
anahisi ni ujanja wa kutaka kuonewa huruma na watu.
Mwendesha mashtaka Gerrie Nel amesema
Pistorius anaanza kujaribu kutumia mchezo wa hisia ambao hata hivyo
hautamsaidia.
Pistorius alikiri kumuua mpenzi wake
Reeva Steenkamp Februari mwaka 2013 kwa kumpiga risasi baada ya
kudhani ni mtu aliyevamia nyumba yake.
Picha juu inaonyesha risasi nne ambazo zilipenya katika mlango wakati mwanariadha huyo alipofyatua na kumuua mpenzi wake
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni