Waziri wa Mambo ya
Ndani wa Ukraine amesema vikosi vya nchi hiyo vimeanzisha operesheni
ya kuwadhibiti wanaharakati wanayoiunga mkono Urusi wanaoshikilia
kituo cha polisi tangu siku ya jumamosi.
Waziri huyo Arsen
Avakov ametangaza kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa vikosi vyote
vya ulinzi vinahusika katika zoezi hilo aliloliita la kukabiliana na
magaidi, Mashariki mwa Mji wa Sloviansk.
Urusi imeonya kuwa
matumizi yoyote ya nguvu dhidi ya wanaharakati Mashariki mwa Ukraine
yataathiri mazungumzo ya mgogoro huo yanayotarajiwa kufanyika baadae
wiki hii.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni