Watu 22 wamelazwa katika hospitali ya Mkoa ya Mbarara nchini Uganda baada ya kudaiwa kula chakula chenye sumu siku ya jumapili ya Pasaka katika Kanisa la Mbarara.
Wahubiri wa Kanisa hilo la Miracle Centre Church wakiwemo watoto na wahudumu wa Kanisa hilo lililopo eneo la Lugazi, walianza kulalamika maumivu makali ya tumbo baada ya kula wali, chapati, matoke, maharage na nyama baada ya misa kanisani hapo.
Muhubiri wa Kanisa hilo, Douglas Kabuye akizungumza akiwa kalazwa hospitalini hapo, alisema chakula hicho kiliandaliwa mapema asubuhi kabla ya misa kisha kikaachwa jikoni kabla ya kuliwa baada ya misa.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni