.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 9 Mei 2014

AJIFUNGUA WATOTO MAPACHA NDEGE IKIWA ANGANI HUKO URUSI

Mwanamke mmoja amejifungua ndani ya ndege wakati ikiwa angani, na amejifungua watoto mapacha, mmoja ndani ya ndege nawa pili mara tu baada ya ndege kutua. 

Mwanamke huyo Irina Vasylkova mwenye umri wa miaka 25, ujauzito wake ulikuwa na miezi 35 wakati anapanda ndege hiyo ya Polar Airline akitokea Zyryanka, mashariki mwa Urusi kuelekea Yakutsk na ndipo alipojisikia uchungu wakati akiwa safarini.
 Mmoja wa wahudumu wa ndege hiyo, Christina Kondratiev ( picha chini ) alipoona hali hiyo na kumjulisha mara moja rubani na kuuliza kama kuna daktari ndani ya ndege hiyo kwa ajili ya kumsaidia abiria huyo, ndipo alipojitokeza Elena Sleptcova mwenye miaka 47 kutoa msaada wa abiria huyo kujifungua salama. 

Mtoto wa kwanza alijifungua angani na pacha wa pili alijifungua mara tu ndege ilipotua. Baada ya hapo wote walikimbizwa hospitali ambako wanaendelea vyema.
                                                    Mhudumu wa ndege hiyo, Christina Kondratiev

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni