Mkurugenzi wa Masoko na Ukuzaji wa Biashara wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Deogratius Kwiyukwa(katikati) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu uzinduzi wa kadi za kisasa za benki hiyo kwa wanachama wa klabu za Simba na Yanga. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga na Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga.
BENKI ya Posta Tanzania (TPB) imeandaa akaunti maalumu kwa ajili ya mashabiki wa Simba na Yanga yenye lengo la kuwatambua na pia kuwawezesha kuchangia klabu zao.
Akaunti hiyo imeandaliwa baada ya viongozi wa pande mbili za klabu hizo kwa kushirikiana na TPB kufikia makubaliano ya pamoja. Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu akaunti hiyo, Mkurugenzi wa Masoko na Ukuzaji wa Biashara wa benki hiyo, Deogratias Kwiyukwa alisema itazinduliwa rasmi Mei 16, mwaka huu Dar es Salaam.
Kwiyukwa alisema kupitia akaunti hiyo wanachama wa klabu hiyo watakuwa wanalipa ada za uanachama kupitia huko, ambapo watakuwa na kadi maalum inayofanana na 'ATM'.
"Benki ya Posta tunatambua tuna mchango mkubwa katika kusaidia michezo ndio maana tumerasimisha kidijitali kuwatambua mashabiki waweze kuchangia klabu hizo na kuziongezea mapato ambayo yatasaidia klabu husika kuwalipa wachezaji mishahara," alisema Kwiyukwa.
Kwiyukwa alisema kwa wanachama wanaotaka kujiunga wanahitajika kufika katika Ofisi za Benki hiyo katika matawi mbalimbali nchini na kujaza fomu maalum za kujiunga na kuwa rahisi kwao kuchangia.
Kwiyukwa alisema kwa wanachama wanaotaka kujiunga wanahitajika kufika katika Ofisi za Benki hiyo katika matawi mbalimbali nchini na kujaza fomu maalum za kujiunga na kuwa rahisi kwao kuchangia.
Alisema wameanza kwa klabu mbili za Simba na Yanga lakini ikitokea kuna nyingine zikapeleka maombi kwenye benki hiyo, zitaunganishwa kwenye mtandao huo.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga na Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga, wote kwa pamoja waliishukuru benki hiyo kwa kuonesha utayari wa kuendeleza mpira wa Tanzania.
Sanga alisema ujio wa akaunti hiyo utarahisisha mambo mengi kwa wanachama, lakini pia watawatambua marafiki na mashabiki kwa urahisi na hivyo, kuomba na kampuni na mashirika mengine kuiga mpango huo katika kukuza soka.
Kwa upande wa Kamwaga, alisema uchangiaji wa akaunti hiyo utasaidia SImba kutimiza majukumu yake kwani katika msimu uliopita ilipata kipindi kigumu kutokana na ukata wa fedha na kuhimiza benki nyingine kuwasaidia katika kufanikisha mipango ya kuendeleza soka.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni