.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 9 Mei 2014

URUSI YAONYESHA ZANA ZAKE ZA KIJESHI, RAIS PUTIN AWASILI CRIMEA

Urusi imekuwa ikifanya magwaride makubwa ya kijeshi katika kuadhimisha siku ya ushindi katika vita kuu ya pili ya Dunia, ambapo jeshi la Urusi ya zamani wakati huo likiitwa Red Army liliyasambaratisha majeshi ya kinazi ya Ujerumani.
 Gwaride hilo kubwa kabisa limekuwa likifanyika katika mji mkuu wa Urusi, Moscow.

Leo Rais wa Urusi, Vladmir Pitin aliwasili Crimea, jimbo lilijitangazia kujitenga na Ukraine na kujiunga na Urusi, jambo ambalo limezua mvutano mkubwa toka kwa mataifa mbalimbali Duniani. 

Akiwa Crimea, Rais Putin alihutubia akiwa katika bandari ya Sevastopol.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni