.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 9 Mei 2014

UTAFITI WAONYESHA WATU WENYE MAHUSIANO YENYE MISUGUANO NA MABISHANO HUFA MAPEMA

Kuwa na misuguano na mabishano ya mara kwa mara na mwenza wako, rafiki ama ndugu kunaweza kuongeza nafasi ya mtu kuwa kwenye hatari ya kufa, hususani kwa wale walio kwenye umri wa ujana.

Wataalam wa Denmark wameeleza katika Jarida la Afya ya Jamii, kuwa wanaume wasio na kazi ambao huwa muda mwingi nyumbani na wenza wao na kujikuta katika misuguano na mabishano wapo katika hatari kufa.

Aidha, kukabiliana na hofu na mahitaji ya familia pia kumehusishwa na idadi kubwa ya vifo vya watu kwa mujibu wa utafiti huo.

Takwimu zinaonyesha wanaume 9,875 na wanawake wenye umri kati ya miaka 36 and 52 waliojikuta katika mahusiano yaliyojaa msongo wanaishia kufariki mapema.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni