.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 8 Mei 2014

ANC KINAONGOZA MATOKEO YA AWALI YA UCHAGUZI MKUU AFRIKA KUSINI

Chama tawala cha African National Congress ( ANC ) cha nchini Afrika Kusini mpaka sasa kinaongoza katika uchaguzi mkuu unaofanyika nchini humo. 

Mpaka kufikia sasa, ANC inaonyesha kuwa baada ya kuhesabiwa kwa zaidi ya asilimia 25 ya kura zilizopigwa, chama hicho kinaongoza kwa asilimia 57.3 ya kura zote, kikifuatiwa na chama cha Democratic Alliance ambacho kimepata asilimia 29.2 ya kura zote zilizohesabiwa mpaka sasa. 
 Chama cha ANC kinaimani kubwa ya kushinda na kuendelea kuongoza Taifa hilo kwa muhula mwingine chini ya Rais wa sasa Jacob Zuma.
Watu milioni 25 wamejiandikisha kupiga kura nchini humo, katika uchaguzi ambao kuna jumla ya vituo 22, 000 vya kupigia kura nchi nzima.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni