Beki wa timu ya soka ya Chelsea, Ashley Cole ametangaza kustaafu rasmi soka la kimataifa baada ya kuachwa katika kikosi cha wachezaji 23 wa timu ya Taifa ya England watakaoshiriki fainali za kombe la Dunia nchini Brazil kuanzia June 12 hadi July 13' 2014.
Beki huyo makini uwanjani, ametangaza uamuzi huo usiku wa jumapili baada ya kocha wa timu ya Taifa, Roy Hodgson kumtangaza beki wa kushoto wa timu ya Southampton Luke Shaw mwenye miaka 18 katika kikosi chake kitakachoelekea Brazil.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni