.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 12 Mei 2014

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA YA MANDERA

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa rsami na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ndugu Ahmed Kipozi mara baada ya kuwasili kwenye Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera iliyoko wilayani Pagamoyo tarehe 10.5.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongozana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera Ndugu Rose Ummy (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ndugu Ahmed Kipozi (kulia) na wageni wengine wakitembelea maeneo mbalimbali ya shule hiyo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatilia jaribio la somo la Fizikia (Hooke’s Law: Inayosema ‘The force needed to extend or compress a spring by some distance is proportional to that distance’) lililokuwa likifanywa na mwanafunzi Mwajuma Mwanankuta wa Kidato cha 4 katika Shule ya Sekondari ya wasichana ya Mandera tarehe 10.5.2014.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera iliyoko Wilayani Bagamoyo wakiimba wimbo wa shule kwa ajili ya kumkariisha Mlezi wa shule hiyo Mama Salma Kikwete alipotembelea shule hiyo tarehe 10.5.2014.
Mke wa Rais na Mlezi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mandera iliyoko wilayani Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani Mama Salma Kikwete akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya shule tarehe 10.5.2014.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni