.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 10 Mei 2014

ATEKETEZA FAMILIA NZIMA KWA RISASI KISA MAPENZI, NAYE AJIUA BAADAYE

 Kijana mmoja mwenye miaka 28, amewapiga risasi na kuwaua watu 3 wa familia moja baada ya kutokea kutoelewana na mpenzi wake na baadaye akajiua yeye mwenyewe kwa risasi. 

Tukio hilo lililotokea huko Kusini mwa California, muuaji huyo aliyetajwa kwa jina moja tu la Raul, alimpiga risasi na kumuua mpenzi wake Marry Ann mwenye miaka 25, kisha akawafuata na kuwapiga risasi Manuela Padila mwenye miaka 52 ambaye ni mama mzazi wa mpenzi wake na kisha aliyekuwa shemeji yake mtarajiwa, Juan mwenye miaka 17. 

Wote walipigwa risasi wakiwa katika vyumba vyao. Baada ya kutekeleza alichokusudia, ndipo muuaji akajigeuzia silaha na kujiua mwenyewe.
April Mejia dada wa marehemu ( pichani ), amesema alipatwa na mshituko mkubwa alipofika nyumbani na kukuta familia yake yote imeteketezwa kwa kupigwa risasi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni