.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 12 Mei 2014

BOKO HARAMU WATOA MKANDA WA VIDEO UNAOWAONYESHA WASICHANA WANAOWASHIKILIA MATEKA

Kikundi cha kigaidi cha Boko Haramu kimeonyesha video ambayo inawaonyesha wakiwa mafichoni kusikojulikana wasichana zaidi ya 200 inaowashikilia mateka tangu kuwateka April 14' 2014 kusini mashariki Borno katika kijiji cha Chibok nchini Nigeria wakiwa shuleni. 
 Kiongozi wa kundi hilo Abubakar Ash Shekawi amesikika katika mkanda huo wa video wa dakika 17 akisema kuwa, watakuwa tayari kuwaachilia huru wasichana hao kama serikali nayo itaawachilia huru wapiganaji wao waliopo magerezani nchini humo. Shekawi amesisitiza kuwa, bila kufanya hivyo katu hawatawaachilia huru wasichana hao.
Kiongozi wa kundi la Boko Haramu, Abubakar Shekawi akiongea katika mkanda huo wa video wa dakika 17 akitoa masharti kwa serikali ya Nigeria kabla ya kuachiliwa huru kwa wasichana hao.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni