Basi la Dar Express likiwa limepinduka.
Taarifa ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, zinasema basi la kampuni ya Dar Express lenye namba za usajili T 580 CFP lililokuwa linasafiri kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea Nairobi nchini Kenya, limepinduka leo asubuhi katika eneo la Msata karibu kabisa na daraja la mto Wami.
Chanzo cha kutokea kwa ajali hiyo, ni kupasuka kwa guruduma la mbele la kushoto la basi hilo.
Katika ajali hiyo, imeripotiwa kuwa abiria wote wametoka salama, na tayari wameshapelekewa basi lingine na wameendelea na safari yao.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni