Jaji anayesikiliza kesi ya mauaji
inayomkabili mwanariadha Oscar Pistorius anatarajiwa kutoa uamuzi wa
maombi ya upande wa mashtaka wa kumtaka mwanariadha huyo kuwa katika
uchunguzi wa akili yake kwa muda wa siku 30.
Ombi hilo la upande wa mashtaka
limekuja baada ya mtaalam wa akili jana kuiambia mahakama kuwa
Pistorius amekuwa akiugua tatizo la kuwa na hofu.
Mwanariadha huyo mlemavu anayetumia
miguu ya bandia amekanusha kumuu kwa makusudi mpenzi wake
mwanamitindo Reeva Steenkamp Februari 14, mwaka jana.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni