.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 13 Mei 2014

MAREKANI KUTUMIA PICHA ZA SETILAITI KUBAINI WALIPO WANAFUNZI WALIOTEKWA NIGERIA

Marekani imebainisha kurusha kifaa cha kunasa picha kutoka angani katika nchi ya Nigeria katika kujaribu kubaini walipo wanafunzi wasichana zaidi ya 200 waliotekwa na wapiganaji wa kundi la Kiislam la Boko Haram.

Marekani pia itasaidia kutoa maumbo ya picha za huduma ya satelaiti ya kibiashara na kwa serikali ya nchi ya Nigeria. 

Hatua hiyo imekuja baada ya kutolewa kwa video za wasichana wapatao 130, ambao Boko Haram wamesema watawatoa kubadilishana na wapiganaji wao wanaoshikiliwa na serikali.

Kundi la Boko Haram liliwateka wanafunzi wasichana hao Kaskazini mwa jimbo la Borno Aprili 14.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni