.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 5 Mei 2014

JAMESON WHISKY YATAMBULISHWA RASMI KATIKA SOKO TANZANIA


Balozi wa Jameson Whisky Afrika Bw Nelson Aseka akitoa maelezo kuhusu kinywaji cha jameson kwa wageni.


Meneja masoko wa Jameson Whisky Tanzania Bw Adam Kawa akitoa maelezo kuhusu uchanganywaji wa Jameson na vinywaji vingine kwa wageni
waalikwa.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw Steve Gannon(kulia) pamoja na Bi Rita Bowen kutoka ubalozi wa Ireland (kushoto)
wakifuatilia kwa makini maelezo kuhusiana na Jameson.

Balozi wa Jameson Afrika Bw Nelson Aseka (kushoto) akitoa maelezo kwa wageni waliohudhuria hafla ya utambulisho wa Jameson Whisky kwenye soko la Tanzania kutoka kulia Bi Irene Kiwia, Meneja masoko wa Jameson Tanzania Bw Adam Kawa, David Shambwe na Bw Emilian Rwejuna.

Meneja masoko wa Jameson Tanzania Bw Adam Kawa akimpa maelezommoja wa wageni Bw Emilian Rwejuna kuhusiana na kinywaji cha Jameson.

Kampuni ya Pernod Ricard ni kampuni kubwa duniani inayoongoza katika uuzaji wa pombe kali, Pernod sasa wameingia katika soko la Tanzania kwa nia ya kupanua soko lao na kuzifikia nchi zote duniani. 

Kampuni ya Pernod Ricard hivi karibuni imetambulisha kinywaji chake cha aina ya Jameson Irish Whisky katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Kaz Kaz kwenye hoteli ya Sea Cliff.

Akizungumza katika hafla hiyo balozi wa kinywaji hicho Afrika Bw Nelson Aseka alisema Jameson ni whisky iliyotengenezwa kwa kiwango cha juu iliyochujwa mara tatu Zaidi na laini mara mbili Zaidi ili kumuwezesha mtumiaji kufurahia kinywaji hicho bila matatizo yoyote.

Nae meneja masoko wa Jameson Tanzania Bw Adam Kawa aliielezea kampuni ya Pernod Ricard kama waongozaji katika soko la pombe kali duniani wanaoongoza kwa uuzaji wa pombe zilizotengenezwa kwa kiwango cha juu sana ili kuridhisha wateja wake. 

“Jameson whisky ni kinywaji kizuri kutumika kwa kuwa hakileti shida yoyote kwa mnywaji na ladha yake ni laini na ya kuvutia kumuwezesha mtumiaji kufurahia kinywaji hiki” Alisema

Adam, aliendelea kusema kinywaji hicho kinafanya vizuri katika soko la Tanzania ndiyo maana wameamua kukitambulisha rasmi ili kuendelea kuwapatia wateja wao nafasi ya kukijua vizuri zaidi.

Katika Hafla hiyo iliyohudhuriwa na watu mbalimbali na hasa wadau wa vinywaji vikali pamoja na waandishi wa habari kulitolewa mafunzo ya jinsi ya kutumia kinywaji hicho, uchanganywaji wake na hata historia yake.

Wahudhuriaji walipata fursa ya kufahamu mambo mengi kuhusiana na Jameson whisky na Pernod Ricard kwa ujumla. 

Pamoja na Jameson Pernod pia ni wauzaji wa vinywaji vingine kama, Absolute vodka, Ballantines, Chivas pamoja na vinywaji vingine vingi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni