Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto amesema kamwe serikali ya nchi hiyo haitatishwa na vitendo vya kigaidi vinayotokea sasa, na Kenya haitaondoa wanajeshi wake waliopo nchini Somalia kusimamia amani.
Ruto ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tu baada ya kutokea milipuko ya mabomu katika mabasi mawili ya abiria na kusababisha vifo vya watu 3 na wengine 86 kujeruhiwa jana jioni jijini Nairobi.
Makamu huyo wa Rais wa Kenya amesema katu hawataondoa majeshi yao Somalia hadi nchi hiyo itakpokuwa salama.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni