.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 11 Mei 2014

JAVIER ZANETTI AAGWA INTER MILAN KWA USHINDI, HUKU HUZUNI IKITAWALA

                         Zanetti akifuta machozi huku akibembelezwa na wachezaji 

Mchezaji Javier Zanetti amecheza mchezo wake wa mwisho katika dimba la San Siro akiwa Inter Milan, mchezo ambao wameibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Lazio hapo jana.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40, ambaye aliichezea Inter Milani michezo 863 aliingia dimbani mnamo dakika 52, akichukua nafasi ya beki wa kulia wa Brazil Jonathan na kushangiliwa mno na mashabiki..

Siku ya Ijumaa, mchezaji huyo raia wa Italia, alitangaza uamuzi wa kujiuzulu kusakata soka baada ya kufanikiwa kutwaa makombe 19 na Inter Milan, ambapo sasa atakuwa Mkurugenzi wa Klabu hiyo.
                                    Zanetti akirushwa juu na wachezaji wenzake
                                        Zanetti na familia yake wakiaga mashabiki
               Shabiki wa Inter Milan akiangua kilio wakati wa kuagwa kwa Zanetti

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni