Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang akiongea huku akiwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ( nyuma yake ), Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ( kushoto ), Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir ( mwisho kulia ) jana jumapili May 11' 2014 Ikulu jijini Nairobi.
Serikali ya Kenya na China zimetiliana saini ya kujenga reli ya kisasa itakayounganisha nchi za Afrika Mashariki ambayo itagharimu zaidi ya shilingi bilioni 327.
Rais wa Kenya, Mh Uhuru Kenyatta aliwaongoza baadhi ya wakuu wa nchi za Afrika Mashariki akiwemo Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini katika kutia saini makubaliano hayo na Waziri Mkuu wa China Li Keqiang jana Ikulu jijini Nairobi.
Ujenzi huo wa reli wa zaidi ya kilomita 609, serikali ya China itagharamia kwa asilimia 85 wakati kiasi cha asilimia 15 kilichobaki kitagharimiwa na serikali ya Kenya.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni