.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 12 Mei 2014

RAFAEL NADAL NA MARIA SHARAPOVA WATWAA UBINGWA WA MICHUANO YA MADRID OPEN

                                              Nishikori na Nadal wakipozi kwa picha

Mchezaji tenesi Rafael Nadal ameshinda taji lake la kwanza katika michuano ya tenesi ya Ulaya iliyochezwa kwenye uwanja wa udongo, wakati maumivu ya mgongo yakimlazimisha Mjapan Kei Nishikori kushindwa kumalizi mchezo huo wa fainali huko Madrid.

Mchezaji huyo wa dunia anayeshika nafasi ya kwanza katika mchezo wa tenisi aliongoza wa seti 2-6 6-4 3-0 wakati Nishikori aliyeongoza seti ya kwanza akishindwa kuendelea na kujitoa.

Mrusi Maria Sharapova amefanikiwa kuondoa hofu na kumshinda Simona Halep wa Romania katika mchezo wa finali za Michuano ya Wazi ya Tenesi ya Madrid na kutwa ubingwa.

Mchezaji huyo aliyewahi kushika nafasi ya namba moja katika mchezo huo alipambana na kushinda kwa seti 1-6 6-2 6-3 na kuongeza rekodi yake ya kutoshindwa katika michuano ya uwanja wa udongo katika michezo 11.
                                          Maria Sharapova akishangilia ushindi wake

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni