Mashabiki wakorofi wa timu ya AFC
Leopards wamevamia uwanja na kupelekea kuvunjika kwa mchezo wao wa
Ligi Kuu ya Kenya dhidi ya Thika United ulichezwa jana katika uwanja
wa Taifa wa Nyayo.
Tukio hilo limetokea mnamo dakika ya
85, wakati Thika United ikiwa inaongoza kwa bao moja kwa bila dhidi
ya AFC Leopards, lililopachikiwa kimiani na Dennis Odhiambo mnamo
dakika ya 10.
Wakati mchezo huo ukielekea kuisha
baadhi ya mashabiki wa AFC Leopards walianza kurusha chupa za maji
uwanjani kabla ya kuvamia uwanjani na kumlazimisha refa Nasur Doka
kumaliza mechi hiyo baada ya kushauriana na wasaidizi wake.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni