.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 11 Mei 2014

MABINGWA NI MANCHESTER CITY LIGI KUU ENGLAND

 Mabao mawili toka katika miguu ya wachezaji, Samir Nasri na nahodha mwenye kifua kipana Vicent Kompany yalitosha kuiongoza Manchester City kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza baada kuifunga West Ham mabao 2-0 katika mchezo wa mwisho wa kufunga pazia la ligi hiyo.
 Manchester City wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani mbele ya mashabiki wao waliokuwa wamefurika huku wanashangilia bila kuchoka, leo walijikuta wakitwaa kombe hilo kwa mara ya pili baada ya miaka mitatu.
 Vijana hao wa kocha, Manuel Pellegrin wamemaliza ligi kuu wakiwa na pointi 86, pointi mbili zaidi ya Liverpool ambayo nayo ilikuwa inaupigania ubingwa huo. Liverpool imemaliza ligi ikiwa na pointi 84 baada ya leo kuifunga Newcastle mabao 2-1 hivyo kumaliza ligi ikiwa katika nafasi ya pili.
 Mashabiki wa Manchester City wakishangilia bila kuchoka wakati wa mchezo huo
Nahodha wa Manchester City, Vicent Kompany akiwa amenyanyua juu kombe la ubingwa wa ligi kuu Uingereza huku akiwa amezungukwa na wachezaji wenzake.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni