Kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha
mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius inatarajia kuendelea leo
baada ya mapumziko ya wiki mbili kwa upande wa mshitakiwa kuwasilisha
utetezi wake.
Wataalam zaidi wataitwa wakati
mwanasheria wa Pistorius akijaribu kupangua hoja za mwanasheria wa
serikali kuwa mwanariadha huyo alimuua kwa makusudi mpenzi wake Reeva
Steenkamp.
Pistorius amekuwa akikanusha kumuua kwa
makusudi Reeva Steenkamp siku ya Valentine mwaka jana kwa kumpiga
risasi akiwa amejifungia msalani.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni