Jaji Mkuu wa Tanzania, Mh Mohamed Othman Chande ( katikati ) akielekea katika ukumbi unakofanyika mkutano wa Majaji wanawake Duniani katika jengo la Mikutano la kimataifa la AICC jijini Arusha.
Mkutano mkubwa unaowakutanisha Majaji wanawake Duniani unafanyika mjini Arusha kuanzia leo.
Rais wa IAWJ, Eusebia Munuo, amesema mkutano huo ni muhimu kwa Tanzania, kwani pia wajumbe wengi watatembelea mbuga zetu za wanyama.
Mkutano huo unaoanza leo, utamalizika May 08, mwaka huu na utahudhuriwa na washiriki zaidi ya 600.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni