.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 7 Mei 2014

LIGI KUU UINGEREZA MAN U YAICHAPA HULL 3-1, GIGGS AWEKA UKOCHA KANDO AINGIA KUONGEZA MASHAMBULIZI

 Kinda, James Willson usiku wa kuamkia leo ameibuka shujaa wa Manchester United baada ya kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1 katika mchezo wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Hull City, mchezo ambao ulichezwa katika uwanja wa Old Trafford.
Kinda huyo alifunga mabao mawili kunako dakika za 31 na 62 kabla ya Robin Van Persie kukamilisha bao la tatu kunako dakika ya 86 ya mchezo huo na kumpa ahueni kocha wa muda wa Mashetani hao wekundu, Ryan Giggs. Bao la kufutia machozi la Hull City lilifungwa na mchezaji Fryatt dakika ya 63 ya mchezo huo. 
Kocha wa muda wa Man U, Ryan Giggs akiingia uwanjani kusaidia mashambulizi. Hapa akiingia kuchua nafasi ya Tom Lawrence kunako dakika ya 70 ya mchezo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni