Mahakama nchini Thailand
imetoa uamuzi wa kumtaka Waziri Mkuu wa nchi hiyo Yingluck
Shinawatra kujiuzulu kutokana na kutumia vibaya matumizi ya madaraka.
Mahakama ya Katiba imetoa
hukumu hiyo kwa kueleza kuwa Bi.Yingluck alikiuka sheria wakati
alipomuhamisha mkuu wa usalama wa taifa wa nchi hiyo.
Uamuzi huo wa Mahakama
umekuja baada ya kuwepo kwa mvutano mkubwa wa kisiasa nchini Thailand
ambapo waandamanaji walikuwa wakiandamana kwa miezi kadhaa kumtaka
Bi. Yingluck kujiuzulu.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni