Mahakama Kuu ya London imeanza
kusikiliza malumbano ya mgogoro wa hati miliki ya nyimbo zaidi ya 13
za mwanamuziki wa Jamaica Marehemu Bob Marley.
Wachapisha nakala za muziki Cayman
Music wanajaribu kupata haki ya nyimbo hizo, miongoni mwao ikiwemo ya
traki ya 'No Woman, No Cry'.
Kampuni hiyo imedai kuwa hawakuhusishwa
wakati zikiuzwa haki za nyimbo hizo mwaka 1992 kwa Blue Mountain
Music, na wakati Bob Marley akitia saini na watu wengine. Hata hivyo
Kampuni ya Blue Mountain imesema nyimbo hizo zilihamishiwa kwao kwa
mujibu wa makubaliano yao.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni