Polisi nchini Brazil wamewataka watalii
nchini humo kuto piga kelele au kufanya jambo lolote lakujihami
wakati watakapokumbana na tukio la shambulizi au uvamizi wa majambazi
wakati wote watakapokuwa nchini humo.
Hiyo ni moja ya dondoo ambazo Polisi
nchini Brazil wameandika kwenye kabrasha maalum kwa ajili ya
kuwakumbusha wataliii nchini humo jinsi gani wanaweza kuishi salama
wakati wa pilika pilika za michuano ya kombe la dunia.
Dhumuni hasa la dondoo hii, ni
kutowafanya majambazi au wanyang'anyi kufanya maafa zaidi kwa
mwathirika wa uhalifu, kwani kupiga kelele au kujaribu kujiokoa
kunaweza kusababisha maafa zaidi.
Wachambuzi wa mambo wamehoji iwapo
dondoo hizi zinampa mhalifu mwanya zaidi wa kufanya uhalifu. Hata
hivyo Polisi hao wa Sao Paolo wamesema ni bora kuvamiwa na kuibiwa
kuliko kuuwawa. Watalii wametakiwa kutokubeba vitu vya thamani hasa
maeneo ya wazi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni