.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 8 Mei 2014

MALALA AJITOKEZA HADHARANI KUPINGA KUTEKWA KWA ZAIDI YA WASICHANA 20 HUKO NIGERIA

Kampeni ya kutaka wasichana wa shule zaidi ya 200 waliotekwa wakiwa shuleni nchini Nigeria waachiliwe huru imezidi kushika kasi, baada ya mwanaharakati maarufu kijana nchini Pakistani, Malala Yousafzai ( pichani ) kujitokeza hadharani na kuomba nchi zote duniani kulaani kitendo hicho kilichofanywa na kundi la Boko Haramu katika jimbo la Borno, nchini Nigeria. 

Malala binti aliyejipatia umaarufu baada ya kutekwa na wapiganaji wa Taliban na kupigwa risasi ya kichwa na kunusurika kifo, amesema kitendo cha wasichana hao kutekwa hakikubaliki na hakivumiliki. 
Mke wa Rais wa Marekani Barack Obama, Michelle Obama akiwa ameshika bango lenye ujumbe wa wa kutaka kuachiliwa huru kwa wasichana hao 
Tayari viongozi wa sehemu mbalimbali duniani wameanza jitihada za kuwatafuta na kuwaokoa wasichana hao, ambapo Rais Barack Obama ametangaza kupelekwa Nigeria kwa kikosi maalum cha wataalam ili kusaidia kuwatafuta na kuwaokoa wasichana hao.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni