Ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza sasa unanukia kwa Manchester City, baada ya timu hiyo inayonolewa na kocha Manuel Pellegrini usiku wa kuamkia leo kuitandika bila huruma Aston Villa mabao 4-0 katika mchezo ambao umefufua tena kwa ari kubwa timu hiyo kuutwa ubingwa msimu huu.
Mabao ya Manchester City yalifungwa na Edin Dzeko katika dakika za 64 na 72, kabla ya Jovetic kutupia bao la tatu kunako dakika ya 89, na bao la nne likiwekwa kimiani na mchezaji mwenye nguvu na mashuti makali raia wa Ivory Coast, Yaya Toure dakika ya 90.
Kwa matokeo hayo, Manchester City imefikisha pointi 83 na kuongoza ligi, ikifuatiwa na Liverpool wenye pointi 81, huku Chelsea wakiwa katika nafasi ya tatu na pointi 79. Mpaka kufikia sasa City wana nafasi kubwa ya kuutwa ubingwa wa ligi kuu msimu huu tofauti na Liverpool au Chelsea.
Mashabiki wa Manchester City wakiwa na bango la kumsifia kocha wao Manuel Pellegrini ambaye toka aanze kuifundisha timu hiyo imeonyesha kiwango cha hali ya juu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni