Ubalozi wa Marekani
umesema makanisa nchini Uganda yapo katika hatari ya kukabiliwa na
mashambulio ya kigaidi wakati huu ambopo Kenya ikikabiliwa na matukio
ya mfulululizo ya milipuko ya mabomu inayofanywa na wapiganaji wa
kundi la al Shabaab.
Taarifa ya Ubalozi wa
Marekani iliyotolewa imesema wapiganaji wa kiislam wanapanga kufanya
mashambulizi katika nyumba za Ibada Jijini Kampala kati ya mwezi huu
ama mwezi Juni.
Taarifa hiyo haijaelezea
kundi lolote linalopanga njama hizo ingawa kundi la Somalia la al
Shabaab lenye uhusiano na al Qaeda limekuwa likilaumiwa kwa
kuhusishwa na matukio kadhaa ya mashambulizi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni