Katika hali isiyo ya kawaida Mke wa rais wa Marekani Michelle Obama ataongea na waandishi wa habari kwa niaba ya mumewe kushutumu tukio la utekaji nyara wanafunzi wakike nchini Nigeria.
Kwa kawaida mke wa rais wa Marekani huwa hajihusishi na mambo ya sera za nje za Marekani, lakini Michelle amekuwa mmoja wa watu wanaopiga kampeni ya kuachiwa wanafunzi hao haraka.
Kundi la Kiislam la Boko Haram limekiri kufanya utekaji huo wa wanafunzi zaidi ya 200, tukio ambalo limelaaniwa mno na watu mbalimbali duniani wakiwemo wakuu wa nchi za magharibi.
Kundi la Kiislam la Boko Haram limekiri kufanya utekaji huo wa wanafunzi zaidi ya 200, tukio ambalo limelaaniwa mno na watu mbalimbali duniani wakiwemo wakuu wa nchi za magharibi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni