Mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Mh Regina Chonjo akizungumza na mmoja wa vijana kati ya vijana 30 wa kata ya Ngunichile ambao aliwahamasisha kujiingiza katika kilimo na kuacha kukaa vijweni. Vijana hao wamefanikiwa kulima shamba la Ufuta lenye ukubwa wa ekari 260.
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Mh Regina Chonjo akiumwagilia maji mche wa Mkorosho katika shamba la Ngunichile ambalo limelimwa na vijana zaidi ya 30. Miche zaidi ya 1,000 imepandwa katika shamba hilo, na hii ni baada ya mkuu huyo wa wilaya kuwahamasisha vijana hao kuacha kukaa vijiweni na badala yake wajishughulishe na kilimo.
Akina mama wa Amandina Saccos wakimsikiliza Mkuu wa wilaya wa Nachingwea, Mh Regina Chonjo ( hayupo pichani ).
Nakagua shamba la vijana wetu!! Mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Mh Regina Chonjo akilikagua shamba la Ufuta la vijana zaidi ya 30 wa kata ya Ngunichile.
Hapa Mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo akihamasisha wanawake kujiunga katika Saccos.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)





Hakuna maoni :
Chapisha Maoni