.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 15 Mei 2014

WANAJESHI NCHINI NIGERIA WAMFYATULIA RISASI KAMANDA WAO

Wanajeshi nchini Nigeria wamemfyatulia risasi kamanda wao Kaskazini Mashariki mwa mji wa Maiduguri.

Meja Jenerali Ahmed Mohammed amefanikiwa kutoka salama katika tukio hilo kwenye gari lake wakati wanajeshi hao walipolifyatulia risasi katika kambi ya Maimalari.

Wanajeshi hao wanamtuhumu kamanda huyo kwa kumuua mwenzao katika shambulio la wapiganaji wanaohisiwa kuwa ni wa Boko Haram.

Wakati huo huo Rais wa Nigeria amekanusha kuwaachia huru wafungwa wa kundi la Boko Haram ili kubadilishana na wanafunzi wasichana zaidi ya 200 waliotekwa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni