.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 7 Mei 2014

MONICA LEWINSKY AFICHUA MAMBO ZAIDI KUHUSU UHUSIANO WAKE NA BILL CLINTON

Monica Lewinsky ameamua kufichua mambo zaidi kuhusiana na kashfa ya uhusiano wake na aliyekuwa rais wa Marekani ambapo amebainisha kuwa alikataa kitita cha dola milioni 10, kutokana na kuona si jambo sahihi kupokea fedha hizo.

Lewinsky aliyekuwa kimada wa Bill Clinton, pia amelieleza jarida la Vanity Fair namna alivyokuwa akikabiliana na mawazo ya kujiua mara baada ya kuibuka kwa kashfa hiyo nzito iliyolitikisa taifa la Marekani mnamo mwaka 1998.

Monica Lewinsky, amekiri kuwa ni kweli rais alitumia ubosi wake kuweza kumnasa lakini hata hivyo uhusiano wao ulikuwa wa maridhiano ya pande mbili, na kwamba alidai kudhalilishwa pale alipotolewa kafara kwa ajili ya kumlinda Clinton wakati wa kampeni.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni