.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 7 Mei 2014

NYOTA WA MAREKANI WASUSIA HOTELI YA THE BEVERLY HILLS INAYOMILIKIWA NA BRUNEI

Nyota wa Hollywood wamegomea kutumia huduma za moja ya hoteli maarufu kutokana adhabu kali za kislam zilizoidhinishwa na serikali ya Brunei.

Nyota hao wa Hollywood Jay Leno na Ellen DeGeneres ni miongoni mwa watu maarufu wanaounga mkono mgomo huo dhidi ya hoteli ya The Beverly Hills pamoja na hoteli zingine zinazomilikiwa na Bruinei.

Baada ya mjadala mkubwa baraza la halmashauri nchini Marekani limepiga kura ya kwa wingi kuishutumu serikali ya Brunei.

Kiongozi wa Brunei, Sultan Hassanal Bolkiah, ameidhinisha awamu ya kwanza ya adhabu hizo ikiwemo ya kuwawa kwa kupigwa mawe kwa mashoga na wazinifu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni