Mtaalam wa magonjwa ya akili ameieleza
mahakama kuwa mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius anatatizo
la kujawa na hofu ya matukio ya uhalifu wa kutumia nguvu tangu
alipokuwa mtoto.
Meryl Vorster amesema kuwa vitendo
vyake vilivyopelekea kumpiga risasi mpenzi wake Reeva Steenkam siku
ya wapendano vilitokana na hali hiyo ya hofu ya uhalifu.
Mwendesha mashtaka sasa ametaka
mwanariadha huyo mlemavu kupelekwa katika hospitali ya wagonjwa wa
akili kwa uchunguzi.
Mwanariadha huyo mlemavu wa miguu yote
miwili amekuwa akikanusha kumuua kwa makusudi mpenzi wake huyo Reeva
Steenkamp.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni