.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 5 Mei 2014

RAIS ZUMA ADAI ILIBIDI KUTUMIA FEDHA NYINGI KUKARABATI NYUMBA YAKE BAADA YA MKEWE KUBAKWA

Rais wa Afrika Kusini Jackob Zuma amesema wahalifu walivunja nyumba yake iliyopo kijijini zaidi ya muongo mmoja uliopita na kumbaka mke wake, katika maelezo yake aliyotoa kujitetea kutokana na matumizi makubwa ya dola milioni 23 ya ukarabati wa nyumba hiyo ili kuboresha usalama.

Maelezo hayo ya rais Zuma ameyatoa wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utakaofanyika Jumatano wiki hii, ambapo ameongeza kuwa wahusika wa tukio hilo la kumbaka mkewe wamekamatwa, kushtakiwa na kuhukumiwa baada ya kufanya uhalifu huo kwenye nyumba yake iliyopo Nkandla KwaZulu-Natal kabla hajawa rais mwaka 2009.

Hata hivyo rais Zuma hakuelezea ni mke yupi aliyebakwa kati ya wake zake wanne ambapo mmoja wao alijiua, na mwingine kutengana naye aitwaye Nkosazana Dlamini-Zuma ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.

Rais Zuma amekosolewa vikali kwa matumizi makubwa ya fedha za walipa kodi, hata hivyo anatarajiwa kushinda uchaguzi mkuu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni